Articles by "Apps"
Showing posts with label Apps. Show all posts
As salaam aleikum ndugu wapendwa wasomaji wa Jukwaa hili ni wakati mwingine tena wa kupeana mawili matatu, wenda imeshawahi kukutokea katika pitapita zako katika mitandao ya kijamii ghafla ukatua facebook ukakutana na video ambayo imekuvutia kisha ukashindwa kuipata kutoka na kutokufahamu jinsi ya kuipakua video hiyo, basi leo nimekuletea njia ya kukuwezesha kuishusha video yeyote kutoka facebook bila usumbufu wowote twende sawa hapa chini nimekuwekea maelezo kamili.

kwanza kabisa pakua App ya Fb Video Downloder hapa

kisha fuata hatua hizi ili kushusha video yeyote
fungua app yako ya Fb video downloder kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa GO TO FB Kisha log in katika facebook akaunti yako
kisha tafuta video unayihitaji kuishusha kutoka facebook kisha iguse au ibonyeze hiyo video
utaona option kama inavyoonekana pichani hapo juu kama unahitaji kuiangalia kabla ya kuishusha bonyeza sehemu iliyoandikwa Stream kama unahitaji kudownload bonyeza sehemu iliyoandikwa download
kama utahitaji kuona idadi ya video ulizopakua kupitia app ya Fb Video Downloader bonyeza sehemu iliyoandikwa Gallery
hapo utaona video zako zote pia zitakuwa zimehifadhiwa katika memory ya simu 
Mpaka hapa utakuwa umeshafahamu jinsi ya kupakua video za facebook kama unaswahili kuhusu makala hii unaweza kuniuliza katika sanduku la maoni nami nitakujibu kwa haraka zaidi Enjoy
UKIANGALIA katika simu yako ni dhahiri Application nyingi ulizopakua ni za bure. Wote tunapenda App za bure.

Mara nyingi App za bure zina gharama ya faragha (privacy) wakati wa kuziingiza katika kifaa chako.

Wengi wetu tumekuwa hatusomi vigezo wakati tunapoingiza App hizo ndani ya simu zetu, huwa tunabonyeza tu ‘agree to continue’ bila kusoma.

Lazima usome kuwatambua waliotengeneza na ujue ni vitu gani unawaachia mikononi mwao kama vile namba za simu, meseji zako, maeneo (locations) na vitu vingine kibao.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na wataalam waliobobea wa kituo cha ESET umebaini uwepo wa Application 29 zilizopo Google Play Store ambazo ni VIRUS aina ya TROJAN

Virusi hao ambao hutumia majina tofauti-tofauti wana uwezo wa kuingilia application zingine zilizopo katika simu yako na kutuma taarifa zote kwa hackers (wadukuzi).

App hizo ambazo zina virus ndani yake, pia zina uwezo wa kutengeneza Fake Logins Page ( Phishing) ambapo ukijichanganya tu, basi taarifa zako za siri kama bank details, email, password (nywila au neno la siri) zako za mitandao ya kijamii huchukuliwa na kutumwa kwa wadukuzi.

Credit : JF
Kampuni ya Yahoo ambayo inajihusisha na utoaji wa huduma za barua pepe, hivi karibuni imetangaza kuja na huduma mpya ambayo itawaruhusu watumiaji wa huduma za Yahoo kuweza kuchat na ndugu na jamaa pamoja na marafiki kwa kutumia huduma mpya inayoitwa Yahoo Together.
Yahoo Together ni app ambayo imechukua muonekano na mtindo wa App ya Slack ambayo pia hutoa huduma ya kuchat kama ilivyo kwenye app hiyo mpya ya Yahoo Together. Tofauti na app ya Slack, App hii mpya ya Yahoo inakupa uwezo wa kuchat kwenye magroup lakini ni lazima kuwa na barua pepe ya mtandao wa Yahoo ndipo uweze kutumia app hiyo mpya.

Moja kati ya sehemu nzuri kwenye app hii ni sehemu inayoitwa Smart Reminders, sehemu hii itakuwezesha kuweka meseji ili ijitume yenyewe kwa wakati fulani na muda huo utakapo fika meseji hiyo itajituma kwa watu wote kwenye group husika. Sehemu nyingine ni Blast, highlights sehemu ambazo zitakupa uwezo wa kuwekea rangi kwenye meseji fulani ili watu wengine kwenye group waweze kuiona meseji husika pale watakapoingia kwenye group.
Kwa sasa tayari app hii ipo kwenye masoko ya Play Store na App Store hivyo unaweza kuipakua moja kwa moja kupitia masoko hayo
Miezi michache iliyopita mtandao wa instagram ulikuwa ukifanya majaribio ya sehemu ya Nametags, sehemu ambayo inakupa uwezo wa kumfollow mtu kwa urahisi kwa kutumia mfumo kama wa QR Code.
Baada ya majaribio ya muda mrefu hatimaye sehemu hiyo tayari imeanza kuwafikia watumiaji wa mtandao huo kupitia App za Android na iOS. Kupitia sehemu hiyo ya Nametags utawezesha mtu kupata akaunti yako kwa haraka na pia utaweza kushiriki na watu akaunti yako kwa namna ya kipekee.


Sehemu hiyo ya nametags inapatikana kwa kubofya sehemu ya mitari mitatu kwa iliyoko upande wa kulia juu kisha chagua nametags, hapo utaona username yako ikiwa na rangi ambazo unaweza kubadilisha kwa kubofya sehemu yoyote kwenye rangi hiyo, pia utaweza kuchagua picha ya selfie, emoji au kuwa rangi mbalimbali.
Kwa sasa tayari tumesha ona sehemu hii kupitia app ya Instagram ya Android lakini bado hatujaona sehemu hii kupitia programu ya Instagram ya iOS, hivyo ni wazi sehemu hii bado inaendelea kutoka na pengine itawafikia watumiaji wengine siku za karibuni.
As salaam aleikum ndugu wasomaji wetu katika ule mfululizo wa Kutengeneza app kwaajili ya kurahisha maisha yetu ya kila siku leo tumekuletea App kwaajili ya mapishi Ingia playstore tafuta Mapishi.

App yetu hii itakurahisishia kupika mapishi mbalimbali ambayo yameandaliwa kwa lugha ya kiswahili bila kusahau Juisi za asili, App yetu hii ya Mapishi ni bure kabisa hakuna kulipia.

app ya Mapishi inakuwezesha kufahamu Mahitaji yote ya pishi unalohitaji kulipika pia unaweza kuforwad au kutuma meseji ya vitu au mahitaji ya mapishi unayohitaji kujifunza ivo unaweza kumtumia sms muuzaji bila hata kunakili sehemu nyingine.

App yetu ya mapishi imegawanyika katika kategori zaidi ya nane kila kategori moja inamapishi ya aina moja kama kama unahitaji mapishi ya aina fulani unaweza kuchagua kategori unayoipenda pia ipo sehemu kwaajili ya mapishi yote, Mapishi App ni rahisi zaidi kuitumia ijaribu sasa hautajutia kuwa na app ya mapishi.

unaweza kuidownload hapa DOWNLOAD hii ni kwaajili ya watumiaji wa vifaa vya android tu
WhatsApp imekuwa ikifanyiwa maboresho karibia kila mwezi, lakini hivi karibuni mabadiliko mapya yanayokuja kwenye programu ya WhatsApp ni ya tofauti kidogo na mabadiliko mengine. Mabadiliko hayo mapya yanahusiana na chanzo cha mgunduzi wa WhatsApp kuamua kuachana na kampuni ya Facebook ambayo kwa sasa ndio inayomiliki programu hiyo maarufu ya kuchat duniani.
Kama wewe ni mmoja wa wafuatiliaji wa tovuti ya Swahili Tech lazima utakuwa umesoma makala juu ya mmoja wa wagunduzi wa WhatsApp kuachana na kampuni ya Facebook na baadae kutangaza kwa wafuasi wake kwenye mtandao wa Twitter huku akiwahitaji wafute mtandao huo.
Sasa kama wewe ni mmoja wa watu ambao walikuwa hawajui sababu ya mgunduzi huyu kusema maneno hayo na kuachana na kampuni ya Facebook basi nitakwambia leo. Miaka kadhaa iliyopita waanzilishi hao waligundua programu ya WhatsApp kipindi hicho kama unakumbuka vizuri njia iliyokuwa inatumika na wagunduzi hao kujipatia pesa ni pamoja na watumiaji kulipia dollar $0.99 sawa na Tsh 2,289 kwa mwaka kwa ajili ya kutumia programu ya WhatsApp.
Mara baada ya Facebook kununua App hiyo sehemu hiyo ilitolewa kabisa na WhatsApp ilibaki kuwa programu ya bure kwa asilimia 100. Lakini sasa hivi karibuni kumetokea kutoelewana kwa Facebook na mwazilishi huyo mweza wa programu ya WhatsApp mara baada ya Facebook kutaka kuanza kuonyesha matangazo kupitia App ya WhatsApp. Kama alivyo hojiwa na tovuti ya Forbes mwazilishi huyo alisema kuwa, mpango wa Facebook kutaka kuonyesha matangazo kwenye App hiyo kunatofautiana na sababu ya wao kuanzisha app hiyo hivyo haoni haya ya kuendelea kufanya kazi chini ya kampuni hiyo inayo kinzana na sababu zake.
Mpango wa Facebook ni kuja na njia mpya ambayo sasa watumiaji wa App ya WhatsApp watakuwa wanaona matangazo kwenye programu hiyo, najua unajiuliza ni sehemu gani matangazo hayo yatakuwa yanaonekana.? Sasa kwa mujibu wa tovuti ya express.co.uk ambayo lithibitsha hayo kwa kufanya mahojiano na mmoja wa wafanyakazi wa Facebook aliandika kuwa, Hadi kufikia mwaka 2019 WhatsApp itakuwa ikionyesha matangazo kupitia sehemu ya Status ambayo inaonyesha video kwa sekunde kadhaa.
Bila shaka kubadilika huku kwa whatsApp kutakuwa ni pigo kubwa sana kwa watumiaji wa WhatsApp, lakini pengine kwa watu wengine hasa wafanyabiashara hii itakuwa ni habari njema kwani sasa wataweza kuwafikia wateja wengi zaidi kupitia programu hiyo.

Kwa sasa bado hakuna taarifa za lini sehemu hiyo itakuja rasmi kwenye programu ya WhatsApp ila mpaka 2019 tegemea kuanza kuona matangazo kwenye programu ya WhatsApp kama ilivyo programu za Facebook na Instagram. Hebu tuambie wewe onaonaje hii imekaa poa au..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

Credit : TanzaniaTech
Wakati mtandao wa Instagram ukiwa kwenye hatua za awali za kuja na programu maalum ya kununua bidhaa kwa kupitia akaunti za Instagram, Kampuni ya Facebook kupitia mtandao wa huo wa Instagram hivi juzi imetangaza kuja na njia mpya ya kuweza kurahisha watu kununua bidhaa moja kwa moja kupitia kwenye app ya Instagram.

Kupitia sehemu ya Stories, Instagram inategemea kuleta sehemu mpya ya Shopping ambayo itakuwa kwenye sehemu ya Explore iliyotambulishwa hivi karibuni ambapo Kupitia sehemu hiyo ya Stories utaweza kuona bidhaa mbalimbali zikiwa zimewekewa stika ambazo utakapo bofya hapo utapelekwa moja kwa moja kwenye tovuti yenye bidhaa uliyo iona kupitia sehemu hiyo ya Stories.
Kama unavyoweza kuona sehemu hiyo kwenye picha hapo juu, pale utakapo bofya sehemu ya Shopping Explore utaweza kuona bidhaa nyingi kutoka kwenye akaunti mbalimbali ndani ya mtandao wa Instagram. Mbali ya hayo pia watumiaji wa mtandao huo watapewa uwezo wa kuuza bidhaa mbalimbali kwa urahisi kwa kuweka stika ya Shopping ambayo itapatikana kwenye sehemu ya Stika kwenye sehemu ya Stories.

Sehemu hii inatarajiwa kuwafikia watumiaji mbalimbali kuanzia siku ya leo hivyo hakikisha unasasisha (update) toleo jipya la App ya Instagram kupitia masoko ya Play Store na App Store.